Header Ads

Breaking News
recent

KAULI YA WAZIRI MWIGULU

TOP STORIES

Kauli ya kwanza ya Waziri Mwigulu Nchemba kuhusu Mwanafunzi Akwilina

on
Leo February 18, 2018 stori inayoshika headlines Tanzania ni kuhusiana na tukio la Mwanafunzi wa NIT kupigwa risasi ambapo Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Dr. Mwigulu Nchemba amemuagiza Mkuu wa jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro na timu ya uchunguzi kutoka jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina juu ya kupigwa risasi kwa mwanafunzi Akwilina Maftah.
Waziri Nchemba ametoa maagizo hayo akiwa mkoani Geita wilaya ya Chato wakati wa uzinduzi wa Gereza la wilaya ya Chato.
Waziri Dr. Mwigulu amelitaka jeshi la polisi kuchunguza kwa kina tukio hilo na kuchukua hatua kwa askari aliyehusika na hilo na kuwaambia wananchi nini kinachoendelea.
“Kama Waziri mwenye dhamana nalaani vikali sana tukio la kupoteza maisha ya binti wetu ambaye hakua na hatia, matukio ya namna hii naona yanaanza kujirudia tena kwa kasi matukio ya kupoteza maisha kwa watu wasiokuwa na hatia hasahasa katika masuala yanayohusu siasa ni mambo ambayo hayakubaliki na ninalaani kwa nguvu zote.” -Waziri Mwigulu
Dr. Mwigulu amewataka wananchi wote kuepuka vitendo hivi vinavyoweza kusababisha madhara kwa namna moja au nyingine na wanapoona matukio ya namna hii watoe ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili wahusika wafikishwe katika vyombo vya usalama.

No comments:

Powered by Blogger.