Header Ads

Breaking News
recent

TOP STORIES: Watanzania Watatu na Wanigeria Watano wamekamatwa na Dawa za Kulevya

TOP STORIES

Watanzania Watatu na Wanigeria Watano wamekamatwa na Dawa za Kulevya

on
February 17, 2018 stori nayokusogezea ni kuhusu Watanzania watatu na raia watano wa Nigeria wanashikiliwa na Idara ya Uhamiaji wakidaiwa kupatikana na dawa za kulevya zikiwamo Heroin, Cocaine, bangi na mashine ya kutengeneza dawa hizo.
Kaimu Kamishna wa Usimamizi na Udhibiti wa Mipaka, Kagimbo Hoseah amesema watuhumiwa wamekamatiwa eneo la Masaki jijini Dar es Salaam.
Hoseah amewataja Watanzania kuwa ni Ruth Kabezi, Lucy Adolf na Lizzy Minja ambaye ni wakili wa kampuni ya Law Associates. Wanigeria wametajwa kuwa ni, Bisola Adeyemi, Olasunkanmi Kayode, Aaron Ejeh, Obina Nwauba na Darlington Nwauba.
 “Tunaendelea na uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi, tutakapokamilisha hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa ikiwamo kuwafikisha mahakamani,” Hoseah.

No comments:

Powered by Blogger.