Header Ads

Breaking News
recent

Waziri Mwigulu atoa agizo kwa wakimbizi


Waziri Mwigulu atoa agizo kwa UNHCR kuhusu wakimbizi

ADTECH GmbH (Master default)
on
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr Mwigulu Nchemba ameliagiza Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR) kuwaondoa haraka wakimbizi 32,000 ambao wameomba kwa hiari yao kurudi katika nchi yao Burundi.
Waziri Dr Mwigulu ameyasema hayo wilayani Ngara alipotembelea kituo cha mapokezi ya wakimbizi cha Lumasi kujionea shughuli zinazoendela katika vituo vya mapokezi ya wakimbizi ambavyo serikaki ilishaagiza vifungwe mara moja.
Dr Mwigulu amesema UNHCR wao wanafanya kazi masaa 24 katika kuwapokea wakimbizi kuingia nchini lakini wanakuwa wazito pale wakimbizi wenyewe wanapotaka kwa hiari yao kurudi kwao baada ya kujiridhisha kuwa kuna amani kwao.
“Tunaanza kupata wasiwasi kuwa mnafaidika na hawa wakimbizi kubaki hapa nchini wakati wao wanahitaji kurudi makwao, naagiza muwaandikie barua leo wakimbizi waliopo katika kambi za Nduta, Nyarugusu na Mtendeli waondolewe haraka sababu hatuwezi kaa na watu ambao wanaitaji kurudi kwao wakajiletee maendeleo” – Dr Mwigulu
Naye mratibu wa wakimbizi kanda ya Kigoma Tonny Laizer amesema kutokana na hali ya usalama nchini burundi pamoja na utekelezaji wa maagizo ya serikali ya kutopokea waomba hifadhi, kituo cha Lumasi kinafungwa na serikali ya wilaya itakabidhiwa na UNHCR kwa ajili ya shughuli za maendeleo

No comments:

Powered by Blogger.