Header Ads

Breaking News
recent

Diamond Platnumz ndani ya Times FM: Ukinifungia nyimbo haunipunguzii kitu nitafanya show hata nje

New
Muda huu Chibu dii Chibu dee anahojiwa sasa hivi kwenye kipindi cha play list kinachorushwa na Times Fm

UPDATES
==========================================

> Siku niliyopewa taarifa za kuimba na ku-perform Kombe la Dunia nilipigiwa simu moja kwa moja kutoka Ikulu nilifurahi sana inawezekana kabla ya kwenda huko nikafanyiwa kitu.

> Tumeanza kuwa na uhusiano na @wema_sepetu kishikaji miaka miwili iliyopita ila watu hawajui tu"

> Nina miaka tisa kwenye muziki ila nikiamua kuzungumza vitu nilivyopitia watu watashika vichwa

> Siogopi kufungwa jela kwa sababu ya sanaa yangu.

Jela zimewekwa na sio wote wana hatia lakini watu wanaenda na Wanatoka,ukweli ni mzuri sana,kama anaelewa atajifunza

> Unaponifungia nyimbo zangu wakati hiyo ndio kazi yangu utanilisha wewe, Tiffah utamnunulia wewe pampers?

> Ukinifungia nyimbo haunipunguzii kitu nitafanya show hata nje.

> Nipo tayar kuhama hata nchi ili nikafanye mziki wangu kwa amani,unaponifungia wakati hauniwekei miundombinu sizani kama ni sawa

> Wanapoongelea maadili na utamaduni wa Tanzania siwaelewi hasa wanataka nini, wakati ngoma za asili za tamaduni zenyewe wengine wanacheza vitovu wazi na kuvaa vibwaya na kubaishiana.

> Kuna vyombo viwili hawapigi nyimbo zangu lakini wafanyakazi wake wananipigia simu wanaomba kufanyakazi kwangu

> Rayvan ana-perfom kwa milioni 10 kwa shoo lakini kuna baadhi ya media wanadhani bila wao sisi hatuendi, zimejaribu kila mbinu na siwezi kufa labla watoke na roho yangu

> Kutokuwa na kiwanja maalum cha kufanyia matamasha ya muziki nchini ni aibu, nina partner alikuwa willing kufanya uzinduzi wa albamu yangu Tanzania lakini imeshindikana, nimefanyia Kenya

> Tunapata project kibao za nje na sasa Hamornize ndiye msanii mwenye fedha kuliko wote WCB”

> Project ya kwanza ya Harmonize niligharamia milioni 39 na ya pili milioni 51, halafu Naibu Waziri haelewi anajua nyimbo zinaimbwa tu, hapo hapo kuna media ikamtaka aka-perform nikakataa wakaanza kumbania,

Times FM

No comments:

Powered by Blogger.