Header Ads

Breaking News
recent

TANZIA: MMLIKI WA MABASI YA SUPER SAMI AFARIKI DUNIA

Mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah maarufu kama Super Sami au mmiliki wa mabasi ya Super Sami amefariki. Ni baada takribani wiki mbili zilizopita alikuwa hapatikani hewani wala kujulikana alipo. Amekutwa amekufa Serengeti na gari lake limechomwa moto.

========

Mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah ametoweka kwa zaidi wiki mbili sasa gari lake aina ya Toyota Landcruizer kukutwa likiwa limechomwa moto katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara.

Gari hilo lililokutwa likitumiwa na mfanyabiashara huyo ambaye ni mkazi wa Mwanza, lilikutwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara jana likiwa limeteketea kwa moto.

Ofisi habari wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa), Mustapha Mwalongo, aliiambia Nipashe kwa njia ya simu kuwa mfanyabiashara huyo licha ya gari lake kukutwa limeteketea moto, hawakukuta mabaki ya mwili wake.

"Gari lake limeteketea kweli lakini hatujabaini mwili kama na yeye alikuwa kwenye gari lile kwa sababu waliofika eneo la tukio hawajakuta mwili au mabaki ya mwili ya aina yeyote", alisema Mwalongo.

Alisema baada ya mmiliki huyo wa mabasi kutoweka tangu Machi Mosi, Kamati iliundwa ya kufuatilia sababu za kutoweka kwake na wapi alipo ambayo inashirikiana na familia.

"Kamati ilipopata taarifa kuwa kuna gari limeteketea kule Serengeti, walishirikiana na Jeshi la Polisi kwenda hadi eneo la tukio na kubaini kweli ni gari lake lakini hawajabaini kama alikuwepo mle wakati linachomwa", alisema Mwalongo.


IMG_20180309_120712_304.jpg

No comments:

Powered by Blogger.