Header Ads

Breaking News
recent

Serikali: Taarifa ya umri wa kudahiliwa kidato cha 5 ilikosewa. Ni kuanzia miaka 25 badala ya miaka 20

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Avemaria Semakafu amefunguka na kuweka wazi utata ulioibuka kuhusu kigezo cha umri wa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita na kusema taarifa ambayo inasambaa imekuwa na makosa.

Semakafu amesema hayo alipoongea na www.eatv.tvna kusema kuwa yametokea makosa ya kiuandishi ila kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita ni miaka 25 na siyo miaka 20 kama ambavyo inasomekana katika taarifa aliyotolewa mapema leo.

"Kumetokea makosa ya kiandishi, miaka ni 25 ya kujiunga sekondari na sio 20 kama ambavyo inasomeka kwenye ile karatasi" alisema Semakafu

Awali ilikuja taarifa ikisema Vigezo vya kujiunga kidato cha 5 mwaka 2018/2019; Mwanafunzi mwenye umri zaidi ya miaka 20 kutodahiliwa


elimu.jpg

No comments:

Powered by Blogger.