Header Ads

Breaking News
recent

MAKONDA: ALIYEDAI KATEKWA AMECHAFUA MKOA WANGU

Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda amesema mwanafunzi anayedaiwa kutekwa, Abdul Nondo ameuchafua mkoa wa Dar na kusema polisi wa Iringa wakimalizana naye wampeleke kwake

Makonda amesema jeshi la polisi limefanya kazi kubwa na hapendi kuona likichafuliwa na watu wachache

Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda amewataka Polisi wa Mkoa wa Iringa wakimaliza kushughulika na mwanafunzi aliyesema ametekwa wampeleke Dar kwa maana ameuchafua mkoa

Aidha, amewataka Waandishi wa Habari waangalie taarifa wanazopeleka kwa umma, kama hazijathibitishwa na mamlaka husika waachane nazo. Amtaka Kamanda Mambosasa na Jeshi la Polisi kutembea kifua mbele, bila ya kuwepo kwa mtu wa kuwafedhehesha wala kuwanyong'onyesha

Makonda amesema "Watu wanahangaika kwenye mitandao ya kijamii kutukana viongozi na kuhamasisha maandamano, nawapa pole sana. Watafanya hivyo labda mie nikiondoka lakini sio nikiwa mkuu wa mkoa". Amemuagiza Kamanda Mambosasa washughulike kwa mujibu wa sheria na mtu yeyote atakayesimama na kutukana viongozi hasaa kiongozi wa nchi ambaye ni Nembo ya nchi

Ameongeza kuwa "amani ya mkoa wa Dar ni muhimu sana na lazima tujue wengine wakipiga kelele wakaandikwa kwenye front page za magazeti ndio wanapata donors kutoka kwa mataifa yasiyotutakia amani"

Februari 26, 2018. IGP Simon Sirro alisema Ole wake atakayeandamana bila kufuata sheria

Mnamo Februari 28, 2018. Mkuu wa Majeshi, Venance Mabeyo alisema Kuna viashiria vinavyotishia Usalama wa Nchi, hatua zinachukuliwa kudhibiti hali hiyo.

Leo Machi 9, 2018 Rais Magufuli amesema Ole wake atakayeandamana, kama kuna baba zao wanawatuma watakwenda kuwasimulia vizuri

Leo Machi 9, 2018. Jeshi la Polisi pia kupitia Mkuu wa Operation na mafunzo, CP Nsato Marijani wakati alipokutana na vyombo vya habari amekionya kikundi kinachohamasisha maandamano ya kuiangusha Serikali kupitia mtandao wa Telegram






For the English Audience Dar es Salaam Regional Commissioner, Paul Makonda has ordered the Police force in Iringa region to hand over to him, Mr Abdul Nondo, a University Student who claims he was abducted on 6th March in Dar es Salaam and found in Iringa on 7th March for scandalizing his region.

Makonda also warned Journalists to be careful about publishing news that hasn't been confirmed by authorities.

He further ordered Dar's Regional Police Commissioner to deal with anyone who dares to insult leaders especially the president who is a National Symbol and insists that whoever wants to conduct demonstrations may do so but not when he is the RC.

Earlier today, President Magufuli warned anyone who wants to participate in demonstrations saying "If they are sent by their fathers, they will give them feedback"

On 28th of February, The Chief of Defense forces, General Venance Mabeyo mentioned that the internet is a threat to national security.

No comments:

Powered by Blogger.