Header Ads

Breaking News
recent

WAZIRI MWIGULI: ABDUL NONDO ALIJITEKA, ALIJIPULIZIA HADI PAFYUMU

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba akiwa anaongea kwenye mkutano wa ziara ya Rais John Magufuli amesema kiongozi wa mtandao wa wanafunzi aliyeripotiwa kutekwa juzi alikuwa amejiteka

Mwigulu amesema kijana huyo alikuwa amejipulizia na pafyum, na kubadilisha nguo na kuuliza alipata wapi muda wa kujiandaa kama kweli alitekwa?

Kauli hii ya Waziri wa mambo ya ndani, ambayo imefuatia kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda imeshahitimisha na kumhukumu kijana huyo ambaye polisi walisema wanafanya uchunguzi kujua kama alitekwa kweli

Polisi hawawezi kuendelea kufanya uchunguzi wa jambo ambalo tayari limeshahitimishwa na bosi wao..Kwa hiyo alipo ananyanyaswa kwa ajili ya kukomolewa pekee

Pengine kijana huyu ametekwa kweli, na Serikali haihusiki kabisa kumteka, ila kutokana na watu wengi kuinyooshea kidole, basi Viongozi wamepandwa na hasira na kumkukumu kijana bila weledi wowote

Kijana huyo bado ameshikiliwa na polisi na amenyimwa kuonana na ndugu wala wakili wake, Polisi wakidai wamemshikilia kama mhanga, na sio mhalifu


No comments:

Powered by Blogger.