Header Ads

Breaking News
recent

MAMBOSASA: ABDUL NONDO ALIKWENDA IRINGA KWA MPENZI WAKE

Jeshi la polisi leo limeongelea uchunguzi wake kuhusu mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam aliyedaiwa kutekwa, Abdul Nondo kwamba alitekwa na watu wasiojulikana, taarifa ambayo ilizua taharuki kwenye mitandao ya kujamii.

Kamanda Mambosasa amesema walifungua shauri la kuchunguza na kubaini ukweli, anasema walipata taarifa kutoka jeshi la Polisi Iringa kwamba mwanafunzi huyo alipatikana Mafinga akiwa salama na kuendelea na shughuli zake na hakuripoti popote kabla ya kukamatwa.

Jeshi la polisi kanda maalumu limesema mwanafunzi huyo hakutekwa bali alijiteka au kuamua kutoa taarifa hizo ambazo zilikuwa na maslahi kwake binafsi, labda umaarufu wa kisiasa kulingana na kujishulisha na mtandao wa kisiasa kwa mujibu wa kamanda Mambosasa.

Mambosasa amesema upelelezi umebaini mwanafunzi huyo alikwenda Iringa kwa mpenzi wake ambae alikuwa akifanya nae mawasiliano mara kwa mara akiwa njiani kuelekea Iringa, baada ya kufanya uchunguzi wa kisayansi wameona muda baada ya kusema ametekwa, simu yake iliendelea kufanya mawasiliano na binti aliemfata.

No comments:

Powered by Blogger.