Header Ads

Breaking News
recent

KUBENEA AFUNGUKA KUFUKUZWA OFISINI NA MKUU WA WILAYA

Fahamu sababu wabunge Mdee, Mnyika na Kubenea kuondolewa ofisi za DC Kinondoni

Kumekuwepo na taarifa inayosambaa kuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amewafukuza kwenye ofisi zake wabunge Halima Mdee (Kawe) na Saidi Kubenea (Ubungo). Baada ya kufanya mawasiliano na DC Hapi ukweli ni huu ufuatao:-

1. Uamuzi wa kuwaondoa wabunge hao ulifanyika katikati ya mwaka jana 2017.

2. Si Halima Mdee na Kubenea pekee walioondolewa. Bali Mdee (Kawe), Mnyika (Kibamba) na Kubenea (Ubungo) wote waliandikiwa barua kuwataka wahame wakipewa notisi ya kujiandaa.

3. Wabunge wote hao walikua hawana ofisi majimboni kwao walikochaguliwa (Kawe,Kibamba&Ubungo)na badala yake ofisi zao zilikua kwenye Jimbo la Kinondoni kwa Mkuu wa wilaya.

4. Uamuzi wa kuwaondoa ulilenga kuwafanya wakatafute ofisi kwenye majimbo yao kwa wananchi waluowachagua mwaka 2015 ili kuimarisha demokrasia.

5. Wabunge wote hao watatu hawakua hata na ofisi za kupanga kwenye majimbo yao hivyo kuwafanya wananchi kupata taabu ya kuwafikia.

6. Hakuna Sheria inayomtaka Mkuu wa wilaya kuwapa ofisi wabunge hao isipokua utashi.Wabunge wengine wana ofisi zao Binafsi.

7. Ofisi walizoondolewa Halima Mdee, Kubenea na Mnyika zilihitajika kwa matumizi mengine ya serikali chini ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi.

8. Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni iko katika Jimbo la Kinondoni.

Huo ndio ukweli wa wabunge hao kuondolewa.

--- Aliyosema Kubenea baada ya kupata taarifa ya kunyang'anywa ofisi---

Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea amesema, mkuu wa Wilaya ya Kinondoni anatafuta sifa kupitia jina lake ili apandishwe cheo, maana wakuu wa Wilaya wote wanaoonekana kuwafanyia uovu wapinzani hupandishwa cheo

Kubenea amefafanua suala la kufukuzwa kwake ofisi na mkuu wa Wilaya huyo kuwa ni uongo kwani ofisi hizo alishazihama tangia muda mrefu, na hivyo mkuu wa Wilaya hana cha kujisifu ili apandishwe cheo na Magufuli


 

No comments:

Powered by Blogger.