Header Ads

Breaking News
recent

Mahakama ya Afrika Mashariki (EAICC) yaiondoa kwa muda kesi ya Uhalali wa Muungano

Majaji katika Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki mjini Arusha wamekubaliana na walalamikaji kuiondoa kesi hiyo kwa muda ili kufanyiwa marekebisho ya kiufundi, kutokana na mapungufu yaliyojitokeza kwenye uwasilishwaji wake.

Akizungumza kwa njia ya simu na Zaima Media akiwa Arusha, mlalamikaji mkuu kwenye kesi hiyo, Rashid Salum Adi anayewakilisha wenzake 39,999, amesema baada ya kesi hiyo kuwasili mahakamani hapo kwa mara ya kwanza na pingamizi za kila upande kusikilizwa na kujibiwa, imekubalika kuwa uwasilishwaji wa kesi hiyo ulikosa mambo ya msingi, ambayo yanahitajika kuwepo.

“Tumefika mahakamani lakini mahakama imekataa kuendelea kulisikiliza shauri letu kutokana na mapungufu yaliyotokea kwetu,” alisema Adi.
Licha ya kushindwa kutajwa kwa kesi yenyewe ya msingi ambayo inahoji uhalali wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Adi aliiambia Zaima Media kwamba kufika kwao kwenye mahakama hiyo na kuwasilikiza wapinzani wao (upande wa serikali zote mbili) kumewasaidia “kuujuwa uzito na wepesi wao na woga wao pia.”

Kwa mujibu wa Adi, wanatazamia kurudi tena mahakamani hapo ndani ya kipindi cha wiki mbili kutoka sasa kurekebisha mapungufu yaliyojitokeza.

“Tuna haki ndani ya wiki mbili kuliwasilisha tena mahakamani, na tunategemea kufanya hivyo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu,” alisema.

- Zaima Media.

No comments:

Powered by Blogger.