Header Ads

Breaking News
recent

RAIS MAGUFULI ATOA ONYO KALI DHIDI YA WAANDAMANAJI

Rais Magufuli amesema ole wake mtu yeyote atakayeandamana siku hiyo na kama ametumwa na baba yake basi atakuja kusimulia vizuri kilichompata.

Rais amesisitiza kuwa nchi hii ni ya amani na kuna watu hawapendi kuona nchi hii inaendelea kuwa na AMANI.

Na nukuu - ''Wapo watu ambao wameshindwa kufanya siasa za kweli wangependa kila siku tuko mabarabarani tunaandamana. Watu wao wanahamia huku wao wanataka wabaki wanaandamane kule. Nimeshasema ngoja waandamane wataniona. Kama kuna baba zao wanawatuma, watakwenda kuwasimulia vizuri. Niliapa kwa Katiba kwamba nchi hii lazima iwe ya amani.''

Ametoa rai kwa wananchi wote kuendelea kuitunza amani iliyopo kuliko kutaka kuingiza nchi kwenye migogoro kama nchi zingine tunazosikia huku mashariki ya kati na hata nchi jirani.

Rais Magufuli ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa tawi la Benki ya CRDB huko wilayani Chato leo hii.



Februari 26, 2018. IGP Simon Sirro alisema Ole wake atakayeandamana bila kufuata sheria

Mnamo Februari 28, 2018. Mkuu wa Majeshi, Venance Mabeyo alisema Kuna viashiria vinavyotishia Usalama wa Nchi, hatua zinachukuliwa kudhibiti hali hiyo.

Leo Machi 9, 2018 Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaonya wale wote wanaotaka kuandamana katika mkoa huo na kuwaambia labda wafanye hivyo yeye asipokuwa mkuu wa mkoa

Leo Machi 9, 2018. Jeshi la Polisi pia kupitia Mkuu wa Operation na mafunzo, CP Nsato Marijani wakati alipokutana na vyombo vya habari amekionya kikundi kinachohamasisha maandamano ya kuiangusha Serikali kupitia mtandao wa Telegram

No comments:

Powered by Blogger.