Header Ads

Breaking News
recent

MKE WA RAIS ALIYESHINDWA KUMUUA MUMEWE MARA 638



February 28, 1959 Meli ya Ms Berlin toka Ujerumani ilitia Nanga katika Pwani ya Havanna Cuba, ndani yake alikuwemo Binti Kigori wa miaka 20 Marita Lorenz ambaye Nahodha wa Meli hii alikuwa ni Baba yake Mzazi mwenye asili ya Ujerumani na Marekani na alimpatia Ajira humo.

Macho ya Rais Mjamaa wa Cuba kwa wakati huo Fidel Castro yalipotua kwa Binti huyu alinasa kimapenzi, wakati huo Castro yeye alikuwa na Umri wa Miaka 33, katika Muono wa kwanza(First Sight) Wawili hawa Walipendana mno na hata baada ya Binti huyu kurudi New York.

siku chache baadae Castro alimpigia Simu na kumuomba arudi Cuba haraka sana...na ariporudi akamuajiri kama Mtumishi wake ndani kwenye Apartment yake Ghorofa ya 74 Hilton Hotel Havanna Cuba! ..hii ni kujisogeza karibu na Mzinga wa Asali.

Katika Mapenzi Mazito ya Wawili hawa, Miezi miwili Baadae Marita Lorenz alishika Ujauzito, lakini Furaha aliyokuwa nayo juu ya Ujauzito huu wa Bwana anayempenda haikudumu,... kuna siku alipokuwa akinywa Maziwa kwenye Glasi alianza kujisikia vibaya, kuumwa na hata ujauzito wake kukomea hapo, Mimba ilitoka, hali yake Mbaya ilimlazimu kusafirishwa mpaka Nchini Marekani kwa Matibabu..je nini kilitokea?

Hapa Wodini New York ndipo picha Kamili ilipoanzia, moja ya Watu waliomtembelea hospitali alikuwa Afisa wa Shirika la Kijasusi la Marekani (CIA),akamwambia " Mipango yote ya Mimba yako Kutoka ameifanya Bwana yako Castro, huyo Mtu ni Hatari kwa Marekani, Tunataka kummaliza kabisa, Upo Tayari kushirikiana nasi?"

Kutokana na Maneno ya CIA Marita aliyaamini na akajiuliza sana kwa nini Carlos alimfanyia Ukatili ule na ndipo akakubali mpango huo wa kummaliza Carlos,na hapa ndipo CIA walipofanikiwa Kumlaghai kwani Mipango yote ya mimba kutoka waliiasisi wao na kuifanikisha bila Castro kujua.

January 1960 Binti huyu sasa alikutana na Afisa wa CIA Frank Sturgis mjini Miami Marekani na akapewa Mzigo wa Vidonge kadhaa vya sumu ambavyo angevitumia Kumuua Castro na akapewa mafunzo maalumu ya namna ya kutekeleza..Kisha akasafiri kwenda Havanna.

Siku ya kutekeleza Mission iliwadia, Marita ambaye vidonge hivyo vya sumu alikuwa amevificha kwenye kopo la Cream ya uso alifanikiwa kuweka vidonge kadhaa kwenye Glasi ya Juice ya Bwana yake na akaibeba kumpelekea...Castro alipokea Glasi ya Juice kwa Tabasamu na Mahaba mazito kisha akaiweka pembeni na kutoa Bastola yake iliyojaa Risasi, hapa sasa Marita Lorenz akiongea na Gazeti la Dily Mail mwaka 2016 anasema :

"Alipotoa Bastola yake nilijua sasa nakufa!, lakini akanikabidhi bastola ile huku akisema, si unataka kuniua?, usihangaike tumia Bastola hiyo hapo Mikononi mwako, unaweza kunipiga Risasi utakazo nami sitaamka daima"...

Niliishiwa Nguvu nikashika Bastola ile nikatoa Risasi zote nikaitupa na tukaishia Kufanya Mapenzi..alijua dhahiri pia nisingeweza kumuua, siku Chache baadae nilirudi New York kwa kuhofia kwamba nikibaki na Castro na kumuua siwezi basi CIA wangeniua Mimi, Nikarudi New York na sikurudi tena Cuba mpaka leo hii"

Siku zinakwenda Mbele Uzee unaingia, Historia zinajiandika,hili lilikuwa ni jaribio moja kati ya majaribio 638 katika Misha ya Fidel Castro,...Marita Lorenz kwa sasa ana Miaka 80 na hakuwahi Kurudi tena Cuba ingawa bado anakiri kwa kimombo kwamba "Fidel Castro is the Love of her Life"......



FB_IMG_1520711050276.jpg

No comments:

Powered by Blogger.